BE FORWARD.JP

BE FORWARD.JP
JAPANESE CAR EXPORTER

Tuesday 16 July 2013

MBOWE AJISALIMISHA POLISI DAR


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa
*Ni baada ya kusakwa siku kadhaa
*Ahojiwa kwa tuhuma za uchochezi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amejisalimisha polisi. Mbowe, alijisalimisha polisi jana saa 8.00 mchana makao makuu ya Polisi Dar es Salaam na kuhojiwa na kikosi maalumu cha makachero wa jeshi hilo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, alithibitisha Mbowe kujisalimisha polisi akiwa amefuatana na mwanasheria, Nyaronyo Kicheere.

“Si kweli kwamba Mbowe amekamatwa, amekwenda polisi mwenyewe. Kama nilivyoeleza kwenye mkutano wetu pale Manzese juzi…Polisi walikwenda nyumbani kwake Mikocheni usiku kwa ajili ya kumkamata hawakufanikiwa.

soma zaidi..http://www.mtanzania.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=8263:mbowe-ajisalimisha-polisi-dar&catid=25:siasa&Itemid=41

No comments: