BE FORWARD.JP

BE FORWARD.JP
JAPANESE CAR EXPORTER

Tuesday 16 July 2013

LUDOVICK NAYE APATA DHAMANA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepatia dhamana mtuhumiwa Ludovick Joseph anayeshitakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare. Lwakatare yuko nje kwa dhamana Juni 10 mwaka huu. Ludovick alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana, jana baada ya kusota rumade kwa zaidi ya miezi minne.

Hakimu Katemana alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 22 mwaka huu na aliamuru mshtakiwa kupatiwa dhamana kwa kuwa alitimiza masharti ya dhamana.

Lwakatare na Ludovick walikubaliwa dhamana baada ya kufutiwa mashitaka matatu ya ugaidi na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kubakiwa na shitaka moja la kula njama ya kumdhuru kwa sumu Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.

Katemana katika kukubali kuwapa dhamana washtakiwa hao pia aliwataka kusalimisha hati zao za kusafiria mahakamani na kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha Mahakama.
SOMA ZAIDI

No comments: