BE FORWARD.JP

BE FORWARD.JP
JAPANESE CAR EXPORTER

Wednesday 17 July 2013

Feza,Oneal waoana



 Katika kazi zilizowapa wakati mgumu washiriki wa Shindano la Big Brother The Chase basi ni kazi ya kuoana ambayo mshiriki kutoka Tanzania Feza Kessy na mshiriki toka Botswana Oneal wao waliamua kufunga ndoa ya kimila.
Oneal alianza kwa kuwatembelea wazazi wa Feza nyumbani kwao na kulipa posa kwa ajili ya ndoa. Kabla ya zoezi hilo Oneal alianza kwa kumuomba Feza kwa pete ya uchumba. Binti huyo alipokubali ndipo ndoa ya kimila ikafanyika.
Akiwa ameambatana na mjomba wake Elikem na Angelo, alikuwa amevalia mavazi ya Kimasai akiwa kama mfalme wa Afrika. Dada wa Oneal alikuwa Fatima na mama yake alikuwa Natasha huku shangazi akiwa ni Annabel aliyemaliza taratibu zote za kindoa.
Mambo yote yalikwenda kama yalivyopangwa kabla baba wa bwana harusi, Sulu alipolipia mahari na wakafanya makubaliano ikiwa ni pombe na vinywaji vingine vilitumika katika kumaliza zoezi hilo.
Mama wa bwana harusi, Natasha alikuwa makini katika kumwelekeza mwanaye namna gani ya kumuongoza binti huyo katika maisha yao, huku dada wa Oneal Fatima akiendelea na kazi zingine. Pia katika jumba la Diamond Hakeem alifanya tendo hilo kwa Cleo na kumuomba kumuoa na Cleo alipokubali ndoa ikafanyika.

SOMA ZAIDI...
 

No comments: