BE FORWARD.JP

BE FORWARD.JP
JAPANESE CAR EXPORTER

Wednesday 17 July 2013

TUSISAHAU VITAMBULISHO VYA TAIFA JAMANI

Nida waanza kuchukua alama za vidole, saini, kupiga picha


Kitambulisho cha Taifa 


Ni katika mchakato wa kukamilisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa, ambapo kila Mtanzania itampasa kuwa nacho.
Dar es Salaam. Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imeanza zoezi la kuchukua alama za vidole vyote kumi, kupiga picha na kuweka saini ya kielektroniki kwa wakazi wa Wilaya ya Temeke tayari kwa kutoa vitambulisho hivyo.
Kaimu Mkuu wa Mawasiliano na Machapisho, Thomas William aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, kutokana na wingi wa watu katika Jiji la Dar es Salaam, zoezi hilo limegawanywa katika ngazi ya wilaya hadi wilaya.
“Hili zoezi tumelianza juzi, tunachukua alama za vidole kumi, kupiga picha na kuweka saini za kielektroniki kwa wakazi wa Temeke, tumeanzia Kigamboni na kutokana na ukubwa wake tumeigawanya kwa kanda saba,” alisema.
  William alisema,  kanda ya kwanza inahusisha mitaa yote katika kata za Kimbiji, Pemba Mnazi, Kigamboni, Vijibweni, Kibada, Mji Mwema, Somangila, Kisarawe 11, Tungi na mitaa ya Mtoni Kijichi, Mgeni nani na Misheni iliyoko katika Kata ya Kijichi.
Alisema, ili kuboresha mwonekano mzuri wa picha kwenye kitambulisho hicho, mwombaji anashauriwa kutokuvaa nguo nyeupe, kijivu, bluu mpauko, pinki na kofia au kapelo wakati wa kupiga picha.
Aidha, William aliwataka waajiri wa mashirika mbalimbali kuwaruhusu watumishi kushiriki katika zoezi hilo siku watakayokuwa wamepangiwa ili kurahisisha zoezi hilo na kuepuka usumbufu wa kurudia eneo.

ENDELEA KUSOMA...

No comments: