BE FORWARD.JP

BE FORWARD.JP
JAPANESE CAR EXPORTER

Tuesday 16 July 2013

Vuta nikuvute kuhusu ubora mafuta ya ubuyu waendelea


TFDA ilitoa taarifa kwamba mafuta ya ubuyu  hayafai kwa matumizi ya binadamu kwa sababu yana kiwango kikubwa cha tindikali ya mafuta aina ya Cyclopropenoic fatty acids.Pia ilisema ili yaweze kukidhi vigezo vya ubora na usalama ni lazima yafanyiwe usafishaji wakati wa usindikaji na kwa sasa nchini hakuna aina ya usindikaji huo

Mratibu wa Chama cha Watabibu wa Dawa za Asili Tanzania (ATME), Boniventure Mwalongo amesema taarifa zilizotolewa hivi karibuni na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TDFA) kuhusu matumizi ya mafuta ya ubuyu zinaweza kuleta madhara kwa jamii kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiyatumia.
Akitolea mfano watumiaji wakubwa  wa mafuta hayo, Mwalongo alisema, wenye magonjwa kama ya moyo na wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wamekuwa wakiyatumia mafuta hayo kwa muda mrefu na kudai yamewasaidia.

Endelea kusoma...http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Vuta-nikuvute-kuhusu-ubora-mafuta-ya-ubuyu-waendelea-/-/1597296/1915274/-/l7bye3z/-/index.html

No comments: