BE FORWARD.JP

BE FORWARD.JP
JAPANESE CAR EXPORTER

Monday 15 July 2013

Lwakatare sasa ahamishiwa Moi


Mkurugenzi wa Ulinzi  na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),amehamishiwa katika Kitengo cha Taasisi ya Mifupa(Moi) baada ya kutolewa katika wodi ya Sewahaji ambayo alilazwa awali kwa ajili ya uchunguzi.
Lwakatare ambaye anasumbuliwa na maumivu ya shingo yaliyosababishwa na kusagika kwa pingili mbili za shingo alifika hospitalini hapo Jumanne ya wiki hii, baada ya kuzidiwa na maumivu usiku wa kuamkia siku hiyo.
Akizungumza wodini hapo jana alisema  alikuwa anasubiri ripoti ya madaktari ambao walikaa kikao cha kujadili tatizo lake na jinsi ya kulitatua hatua za awali zilizochukuliwa na kikao hicho ni kuhamishiwa kitengo cha mifupa Moi.


Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, jana, kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya Shingo

No comments: